Shirika la Standard Group kwa ushirikiano na hazina ya kitaifa ya bima hospitali NHIF limezindua mpango wa kuwapa wauzaji gazeti fursa ya kujiunga na wanaochangia na kufaidi mpango wa bima ya hospitali wa hazina ya NHIF. Wakizindua mpango huo katika majengo mapya ya the Standard Group Centre mkurugernzi mkuu wa NHIF BW Steve Kerrich na naibu mwenyekiti wa shirika la Standard Group Paul Melly waliwataka wauza gazeti kuchukua jukumu hilo kuhakikisha kwamba wanajisajili na kuingia katika mpango wa bima ili kuwarahisishia mzigo wakati wanapougua wao wenyewe pamoja na familia zao.


standard;nhif;