Hali ya wasiwasi na taharuki imetanda katika wilaya ya transmara ya masahariki baada ya jamii mbili kuvurugana. Taarifa zinaarifu kuwa jamii hizo zimejihami kwa silaha aina ya bunduki, huku utawala ukishindwa kutatua uhasama baina yao. zaidi ya watu mia nane wamepoteza makazi yao kutokana na vurugu hizo,baada nyumba zao kuteketezwa.inadaiwa wachochezi wakuu wa uhasama huo ni viongozi wa kisiasa maeneo hayo,wakizozania rasilmali za eneo hilo.


Mzozo Transmara