Waziri wa Elimu Fred Matiang'i amewaagiza wakuu wa shule za umma kutowasajili wanafunzi kutoka shule ambazo zimeteketezwa siku za hivi karibuni.  Matiang'i amesema hatua hiyo itasaida kuhakikisha wanafunzi waliohusika kwenye uharibifu wa mali katika shule zao wanawajibishwa. Amesema sharti wahusika wawasilishe barua kutoka kwa wakurugenzi wa elimu kwenye kaunti zao kabla ya kuruhusiwa kusajiliwa katika shule yoyote ile. Wakati uo huo amewataka wanafunzi kutafuta njia mbadala za kuwasilisha malalamiko badala ya kuharibu mali shuleni. Vilevile ametoa makataa ya hadi Jumatano kwa wakuu wa elimu katika maeneo ambayo shule zimeteketezwa kuandaa ripoti kuhusu vyanzo vya visa hivyo. Ameyasema haya baada ya kuizuru Shule ya  Tengecha na ile ya Itierio ambazo mabweni yaliteketezwa na wanafunzi.

Na, Beatrice Maganga


fred matiang’i