Photo: Courtesy

Kuna watu wengine hata ukifanya nini watabonga bila hata kufikiria.

Hata kama umefanya kitu positive bado utawaskia wakiongea tu.

Sijuangi kama hiyo ndio talent yao ama ni kupenda wanapendanga kuongea juu ya watu.

Kitu ikifanyika kwa kijiji hao ndio wa kwanza kujua. Mara mob utapata watu kama hao wanajua mob kuhusu wengine hata kuliko mwenye story.

Akipigiana story yako anaipiga ni kama anakujua kuliko venye wewe unajijua. Anyway, kama mtu talent yake ni kuroroa lazima afanyishe talent yake job.

Unapata couple fulani wamebarikiwa na mtoto, then hii raiya ya kubonga mob inakuja kuona mtoi then wanaanza kusengenyana.

Unaskia, “Umeangalia huyo mtoto vizuri? Nimeona ni kama huyo jamaa alienjoyiwa na bibi yake.

Huyo mtoto hakuna mahali ameshika sura ya baba, sura ni ya mama tupu!”

Eti huyo jamaa anafaa achanuliwe aambiwe mtoto sio wake. Unaskia hawa watu wakuongea wanasema mtoi ana sura ya jamaa wao wa kazi.

Unashindwa jamaa walikuja kukupongeza ama kuchambua sura ya mtoi ndio waseme mtoi babake ni nani. Wanasahau ajuae baba wa mtoto wake ni mama ya mtoto. Lakini juu walipewa hio talent ya kuongea, watabonga tu.

Raiya wanabonga mpaka kijiji inawapatia jina, mara wanaitwa ‘pita usemwe sacco’ juu ukipita ni lazima wabonge kukuhusu.

Mara mwingine akipita wanawachana na maneno yako wanaanza kubonga kuhusu huyo mpita njia mwingine eti, “Hiki ni kile kimtoto kya kile kimama waliachana na bwanake kikaolewa na mwizi.

“Naskianga hikyo kimwizi kikisanya kinapelekeanga hikio kimama kila kitu, yeye ndie huhesabu pesa ya wizi na kuekea waizi bunduki”.

Yani wanabonga kuhusu mtu na saa hizo huyo mtu hajawahi wachana na bwana yake na hajawahi olewa na mwizi ama hata kushirikiana na mwizi! But wabongaji juu job yao ni hio na ni job bila mshahara watabonga tu. Sio poa kuongea negative kuhusu mtu na humjui.


Radio presenter Mbusii;Story za mtaa