Bunge la Kitaifa Jumanne hiii linatarajiwa kurejelea vikao vyake ambapo shughuli ya kwanza ni kuchaigua Kamati ya Uteuzi ambayo itawahoji watu 585 wanaolenga nyadhifa za makatibu Jumatano.

Idadi hii ya watu 585 iliafikiwa baada ya watu zaidi kuongezwa katika orodha ya waliotuma maombi.

Zaidi ya watu 9,000 walituma maombi wakilenga kujaza nafasi za makatibu wa wizara.

Kamati ya uteuzi itakayoteuliwa na Tume ya Huduma za Bunge, PSC inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Kiongozi wa Wengi bungeni, Kiongozi wa waliowachache na wanachama wengine wasiozidi 11.

Mrengo wa Kenya Kwanza utakuwa na makatibu wa wizara 49 ambao wataongoza idara za serikali katika wizara 22.

Wizara 6 zikiwa Uchimbaji Madini, Biashara, Elimu, Ardhi, Barabara na Masuala ya Ndani huku Wizara ya Ulinzi ikiwa na katibu 1.

Wizara nyingine 14 zitakuwa na idara mbili kila moja huku Waziri mwenye mamlaka akiwa na idara moja ya serikali itakayounganisha shughuli za serikali na katibu mmoja.


bunge Kimani Ichungwa Opiyo Wandayi