Hatua ya Kenya kutoitambua Jamhuri ya Kidemokrasi ya Sahrawi kuwa taifa huru inaendelea kuibua mjadala wa kidiplomasia kuhusu uhusiano wake na taifa hilo la Magharibi ya Sahara.

Aidha linaibua maswali chungu nzima kuhusu iwapo Rais William Ruto ameanza vibaya ama la katika uhusiano wa kimataifa. Taifa hilo linalopakana na Morocco limekuwa katika mzozo wa muda mrefu kuhusu mpaka kwenye eneo la Magharibi ya Sahara baada tu ya kujitenga na Morocco na kujitangazia uhuru.

Awali likiitwa Polisario Front, taifa hilo lililotawaliwa na Uhispania lilivamiwa na vikosi vya Morocco vilevile vya Mauritania miaka ya 75 kufuatia mkataba wa kujiondoa wa Uhispania kwenye eneo hilo na kuliachia huru.

Katika kipindi hicho Sahrawi ilijitangazia uhuru kutoka kwa wakoloni wa Uhispania kisha mikataba kadhaa ya amani ikaanza kutiwa saini kati ya mataifa ya Mauritius na Morocco kwenye taifa hilo, mikataba iliyohusu kuondoa majeshi.

Hata hivyo licha ya juhudi za Umoja wa Mataifa kutaka kufanya kura ya maoni kwenye eneo hilo kuhusu uhuru wa taifa hilo, hadi sasa haijafanyika, hali ambayo inaendelea kuifanya Morocco kuzidi kuwa katika mgogoro na Sahrawi.

Katika juhudi hizo zote, Kenya na mataifa mengine Barani Afrika yamekuwa yakishinikiza uhuru wa kujitawala kwa Sahrawi hasa baada ya Umoja wa Afrika AU kulitambua.

.

Keep Reading

Mwaka 2014, mwaka mmoja tu baada ya kuapishwa, Rais Mustaafu Uhuru Kenyatta aliipa idhini Sahrawi kufungua ubalozi wake hapa Nairobi hatua ambayo ilianza kuimarisha uhusiano wa taifa hilo na Kenya.

Japo bado upo mzozo baina yake na Morocco, ni mataifa 41 tu wanachama wa Umoja wa Mataifa UN yanaitambua Sahrawi kuwa taifa huru, hivyo kuuweka uamuzi wa Rais William Ruto wa kutolitambua taifa ambalo AU yenyewe inalitambua kuwa huru kikamilifu katika maswali mengi.

Hata hivyo leo hii, Rais Ruto amesema atashirikiana na UN katika kutafuta suluhu ya mzozo baina ya Morocco na Sahrawi


William Ruto Kenya Sahrawi