Na Suleiman Yeri?

Serikali ilikuwa na taarifa za kijasusi kuwa kundi gaidi la AL-Shabaab lilikuwa likipanga kushambulia  mji wa Mandera lakini taarifa hizo hazikutosheleza kuchukua hatua madhubuthi. Haya ni kwa mujibu wa Msemaji wa serikali Eric Kiraithe.

Akizungumza kwenye kikao na wanahabari Kiraithe amethibitisha kuuliwa kwa watu sita na kundi gaidi la Alshabab katika mtaa wa Bulla Public Works mjini Mandera.

Kiraithe amesema  idadi ya washambulizi kwa sasa haijajulikani, huku akisisitiza kuwa maafisa wa usalama walifika  haraka kwenye eneo la tukio hilo na kuokoa watu waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya kupangisha.

Aidha Kiraithe amesisitiza licha ya kuwapo taarifa za ujasusi ni sharti wakenya wapige ripoti wanapoona mienendo ya kutilia shaka.

 


Eric Kiraithe;Mandera;AL-Shabaab