Maisha ni safari. Safari hii huleta tabasamu katika sura zetu pale tunapokuwa na uhusiano mzuri baina yetu na binadamu wenzetu.
Hata hivyo, tofauti nyingi hujitokeza baina yetu na hata kukwaruza uhusiano tulionao na wenzetu. Vita na mvutano hujitokeza tunapoishi na binadamu wenzetu, wawe ni familia ama hata marafiki.Na iwapo umekumbana na mambo haya, basi wafahamu fika kuwa sio rahisi kuishi na binadamu.
Wengi watakubaliana nami kuwa, wakati mwingine, ni bora kushi na myama wa nyumabani kama vile paka, mbwa na farasi kuliko binadamu.
Sababu ni kuwa wanyama hawa, mara nyingi, hufanya utakavyo. Watu wawili, ama kikundi cha watu wanapowekwa pamoja, iwe ni katika shughuli za kazi au hata katika ndoa, ni nadra sana pasiwe na kukosana. Kwa kifupi, binadamu hukosana, na hili ni jambo la kawaida.
Muhimu ni jinsi tunavyojibeba pale tofauti zinapoibuka kati yetu. Jambo hili ni muhimu kwani maisha, na hata uhusiano baina yetu ni lazima iendelee hata tunapokosana. Siri hapa ni kuvumialiana. Usiwe mtu wa kuchukizwa kila mara unapokosewa.
Kwa mfano niliwahi kuishi na mtu fulani ambaye hakuwa na heshima mezani.
Mara nyingi angezumgumza huku chakula kikiwa mdomoni. Mara nyingine angechekena na kutuonyesha chakula mdomoni. Kuepuka haya, ningetafuta sababu ya kukosa kuandaa meza ya mlo pamoja naye ili nisije nikachafuka roho. Na kwa kuwa singeweza kumfukuza kwani alikuwa na jukumu muhimu katika shughuli zetu za kikazi, ilinibidi kuvumilia huku nikitafuta jinsi ya kumrekebisha.
Kwa kweli baada ya muda wa kumvumilia, na pia mazungumzo hapa na pale, aliweza kujirekebisha.
Huenda mavazi, matamshi au hata kujibeba kwa mtu ikakukoseha furaha, lakini usiwe mwepesi wa kukasirika huku ukiwakasirikia. Usiwachukie watu kwa sababu wana tabia ambazo hazikupendezi, bora uwavumilie huku ukijaribu kuwarekebisha.
Muhimu zaidi, ni pale wapendanao, katika ndoa, wanapochosana. Lazima uwe wavumilivu ilikuisaidia ndoa yako. Kumbuka, huenda mwenzako ana kasoro, lakini, umejiuliza kuhusu nguvu zake? Ni ngapi mazuri ameyatenda? Je, umejaribu kumrekebisha kwa amani na upendo?
Wasiliana nami
annnjambi@yahoo.com