Na, Carren Omae

Mipango ya kubuni rasmi chama cha jubilee yafikia upeo

Mipango ya kuvijumulisha vyama vyote vinavyounda Muungano wa Jubilee ili kuwa chama kimoja imefikia kilele. Hatua hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukabithibiwa vifaa vya chama hicho. Kamati maalum iliyotwikwa jukumu la kuviweka pamoja vyama hivyo na kuwasilisha mipangilio na mapendekezo yake, imempa Rais Kenyatta katiba ya muda, sheria za chama, sheria za uchaguzi za chama na wanachama wake. Mkutano kwa kwanza umeandaliwa katika Ikulu na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na wanachama wa kamati hiyo maalum huku mipango ya kukizindua chama hicho mwezi Septemba ikiendelea. Akizungumza alipokabidhiwa vifaa hivyo Rais Uhuru Kenyatta amesema chama hicho kitazingatia demokrasia na vile vile kuwahusiha wakenya wote. Amesema maafisa wa vyama tanzu watashikilia nyadhfa mbalimbali kikaimu hadi pale chama hicho kitakapofanya uamuzi rasmi kuhusu maafisa wake wakuu. Tayari jumla ya vyama KUMI NA VITATU vimetia saini kujiunga na Jubilee kufikia sasa