Na Carren Omae
Wakenya watalazimika Kugharimia zaidi baada ya Tume ya Kuthibiti Kawi Nchini, ERC kutangaza bei mpya za mafuta.
Kwenye tangazo lake leo hii, bei ya mafuta ya Petroli imeongezeka kwa shilingi 6.76 kwa lita , bei ya mafuta ya Disel imeongezeka kwa shilingi 9.53 kwa lita huku mafuta taa yakiongezeka kwa shilingi 3.41 kwa lita.
Hatua hii inamaanisha kwamba jijini Niarobi lita moja ya Petroli itanunuliwa kwa shilingi 92.93 kwa lita, Disel shilingi 83.24 huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 61.45 kwa lita.
Kwenye taarifa yake ERC imesema kuongezeka kwa bei hiyo kunatokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta ghafi yanayoagizwa kutoka mataifa ya nje. Vile vile kuongezwa kwa ada inayotozwa mafuta katika bajeti ya mwaka 2016/2017