Na Sophia Chinyezi

Hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Isaack Hassan ametekeleza tishio lake la kumshtaki Mhasibu Mkuu wa Serikali, Edward Ouko kufuatia ripoti yake maalumu kuhusu ununuzi wa vifaa vya kupigia kura kwa njia ya elektroniki - BVR wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013.

Hassan amerejea katika Mahakama Kuu kulalamika kwamba Ouko hakufuata maagizo aliyopewa na Jaji Isaac Lenaola mwaka mmoja uliopita, kumtaka aondoe sehemu ya ripoti hiyo ambayo inamhusisha na sakata hiyo. Hassan anamtaka Jaji Lenaola kumshinikiza Ouko kuwasilisha ripoti iliyofanyiwa marekebisho kwa Kamati ya Bunge ya Uhasibu na kufafanua ni kwa nini anahisi kwamba hafai kushtakiwa kwa kukiuka agizo la mahakama.

Jaji Lenaola amempa Ouko hadi Julai 19 kujibu mashtaka hayo.