Baada ya kuangazia wanaume waliojitokeza hapo jana katika makala ya kwanza ya kisunzi cha ndoa na kukiri kudhulumiwa na wake zao,suala kuu linalojitokeza ni kuwepo kwa matatizo ya kijamii yanayotishia umoja wa ndoa na uwiano wa mume na mke. Kusambaratika kwa jamii kukionekana dhahiri kwani wanaume wengi katika mkoa wa kati wameingilia pombe aidha kusahau shida zao. Wengine hata hivyo wanahisi kuwa serikali kupitia wizara ya jinsia imesahau wanaume na kuwainua sana wanawake kiuchumi ilhali wote waume na wake wana matatizo ya kiuchumi.