Imetimia miaka mine,tangu mji wa naivasha kukumbwa na kima cha juu cha ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007. Ni ghasia zilizoumulika mji huo na kuupa sura tofauti kinyume na utulivu uliokuwepo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2007. Na miaka 4 baadae,ali manzu amezuru naivasha kutaka kujua mabadiliko yalioko hususan mwaka huu wa uchaguzi na fikra za wenyeji kuambatana na siasa mjini naivasha.