Mtazamaji, taarifa tuliyoangazia hiyo jana ya mwanamke mwenye aina sugu zaidi ya kifua kikuu na inayotajwa kuwa hatari zaidi na ghali kutibu, kumeibua wasi wasi mkubwa miongonni mwa wakenya, masuali mengi yameibuka ya ni wengine wangapi wanaougua na ambao yawezekana wanaendeleza maambukizi bila kujua? Na iwapo wako, hii inatosa afya ya umma kwenye hatari kubwa. Tunafuatilia taarifa hiyo katika makala ya afya yako, ambapo damaris kitavi anatujuza mengi kuhusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya maradhi ya kifua kikuu, na matibabu yaliyopo.