Tarehe ya leo 13 januari itasalia kama siku muhimu iliona idara ya mahakama ikitoa uamuzi mwingine muhimu kuhusiana na lini wakenya wataanda uchaguzi mkuu. Hisia tofauti zimeibuku kuhusu uamuzi wa mahakama kuweka uchaguzi kufanywa mwezi machi 2013, siku 60 baada ya kumalizika kwa muhula wa miaka mitano wa bunge la kumi, ikiwa vinara wawili wa serikali ya muungano hawatauvunja muungano huo mapema. Pia kuna wasiwasi vipi suala la muhula wa rais kibaki unaomalizika desemba 31 utakabiliwa, huku wengine wakidai kutakuwa na pengo hata hivyo jaji issac lenaola na wenzake david majanja na mumbi ngugi wamepuuzilia katika maamuzi yao kuambatana na sheria za katiba.