Afisa mmoja wa kikosi cha polisi amefariki na wenzake wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya bomu la kuzikwa ardhinilinalodaiwa kuwekwa na wanamgambo wa Al shabab kulipuka huko Hagadera katika kambi ya Daadab. Bomu hilo linasemekana kufukiwa kando kando mwa barabara . Kisa hiki kimejiri wakati ambapo mashambulizi sawia na haya yamekuwa yakishuhudiwa katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Garissa, Wajir na hata Mandera huku uvamizi huo ukidaiwa kutekelezwa na wanachama wa kundi la Al shabab.


Police man killed in Daadab attack