Mabao 16 zilifungwa katika mechi mbili pekee za ligi ya magongo humu nchini. Klabu ya wanawake ya Vikings ilimimina mabao zita dhidi ya timu ya chuo kikuu cha Multi-Media ilhali timu ya wanaume ya jeshi la wanamaji wa Kenya walipata mabao 10-0 dhidi ya Nairobi Gymkhana. Mechi hizo zilichezwa katika uwanja wa city park hapa jijini Nairobi.