Afisa mmoja wa utawala amewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili katika baa moja lililoko katika eneo la Dagoreti. Mashahidi wanadai afisa huyo aliwafumania watu hao na kuwapiga risasi baada ya kupandwa na mori alipofurushwa na meneja wa baa hiyo alipozua vurugu.nduguye marehemu anadai kuwa mwendazake alikuwa mlemavu na alikumbana na kifo chake alipokuwa akijificha kwenye kibanda kinachopakana na baa hiyo baada ya afisa huyo kuanza kufyatua risasi kiholela.tayari afisa huyo ametiwa mbaroni huku uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ukiendelea.


Bar shoot out Dagoretti - Swahili