Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta imetoa idadi ya waliofariki hospitalini humo kutokana na mkasa wa moto huko kitongoji cha sinai kuwa watu wapatao thelathini na saba. Kulingana na daktari Loice Kahoro wa kitengo cha wagonjwa wa mikasa ya kuchomwa au kuungua, waliofariki waliathirika kwa kiasi kikubwa na hivyo kuna haja ya wakenya kutahadhari wakati moto umelipika mahali.