Jaffer Isaak ni miongoni mwa wengi ambao wamejitokeza kuwania wadhifa wa urais . Jaffer aliye na umri wa miaka 38, amezaliwa na kukulia katika mji wa Moyale anatuelezea mengi kuhusu maisha yake ya taabu aliyoyapitia siku zake za ujana kutokana na ufukara uliokuwa umezingira familia yake , Jaffer amewahi kuwa dereva wa teksi nchini uingereza , na pia alihudumu kama mwanajeshi takriban miaka kumi humu nchini . Kwa sasa anajivunia kuishi maisha ambayo sio ya kuhangaika licha ya pandashuka nyingi maishani na ndiye anayetupambia makala ya darubini usiku wa leo.