Changamoto za kuimarisha kiwango cha sukari humu nchini ikiwemo wenye viwanda kuhitajika kuwekeza kwenye teknolojia pamoja na kubinafsisha viwanda vyao ni mojawapo ya malalamishi ya yanayowakera pakubwa wakulima wa miwa. Aidha wakulima wanalalamikia kukandamizwa na hatua ya makampuni ya kusaga sukari kukosa kutii sheria zinalinda maslahi ya wakulima kama vile kuhitajika kupima uzani wa miwa shambani punde baada ya kukatwa badala ya kufanya hivyo katika kiwanda. Kwa mengi zaidi huyu hapa Isabella Kituri katika jitimai la sukari sehemu ya pili.


Jitimai la sukari 2