Kijakazi mmoja anayefanya kazi nyumbani kwa waziri mkuu raila odinga amepatikana akiwa amefariki akiwa chumbani mwake kwenye makaazi wa waziri mkuu. Kulingana na maafisa wa polisi mwanamke huyo alifariki usiku wa kuamkia leo baada ya kupumua gesi ya carbon monoxide kutoka jiko alilokuwa akiota moto kuzuia baridi.