Mahakama kuu imedinda kutoa mwelekeo wowote hadi siku ya jumatatu kuhusiana na agizo la ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka kuwahamisha Chris Okemo na Samuel Gichuru kutoka humu nchini hadi jiji la Jersey kujibu mashtaka ya ufujaji na kuficha pesa ambazo asili yake na kuhifadhiwa kwake nje ya nchi ni kitendawili kikubwa . Mkurugenzi wa mashtka Keriako Tobiko alielekeza maafisaa wa idara ya mashtaka humu nchini kuanza shughuli ya kuwahamisha wawili hao pamoja na kupata ilani ya kukamatwa kwao kwa mengi zaidi tunaungana na mwanahabari Anne Ngugi


Tobiko extradition orders