Na tukiendelea na makala hayio ya mzozo wa umiliki wa ardhi, wenyeji wa maeneo ya chembe kibabamshe na kilifi jimba huko malindi wanatishia kuchukua hatua mikononi mwao, iwapo serikali haitaingilia kati kutatua mzozo wa ardhi uliokumba eneo hilo. Wenyeji wanadai wawekezaji wa kiitaliano pamoja na matajiri wengine wamefika eneo hilo na kuwapokonya ardhi yao kupitia njia zisizo halali. Sasa wengi wamejipata bila ya makao, huku wakidai kwamba wageni ndio wanaofaidika na ardhi hiyo iliyopakana na ufuo wa Pwani.