Shirika la Marekani la maendeleo ya nchi zinazoendelea usaid limeorodhesha taifa la Kenya kama linaloongoza kwa dhuluma na ukosefu wa heshima kwa akina mama wanapojifungua katika vituo vya kimatibabu vya umma, kupitia matusi na vitisho. Shirika hilo limeanzisha uchunguzi utakao gharimu dola milioni moja nukta mbili, unaotarajiwa kutoa mikakati itakayopunguza visa vya dhuluma dhidi ya wanawake wakati wanapojifungua damari kitavi amezungumza na akina mama kadhaa kuhusiana na masaibu wanayopitia akina mama, na taarifa zao ni za kuvunja nyoyo.