Shirika la Uingereza- DFID ambalo limekuwa likifadhili mpango wa elimu ya msingi bila malipo humu nchini sasa limesitisha kufanya hivyo kupitia kwa serikali ya kenya , na badala yake limeamua kuzifadhili shule husika moja kwa moja. Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo humu nchini alistair fernie ambaye amesema kwamba hatua hiyo imechangiwa na serikali ya kenya kutoonyesha uwajibikaji baada ya shilingi zaidi ya milioni mia tano kufujwa katika wizara ya elimu