Wengi watailaumu teknologia na kisingizio cha 'kwenda na wakati' kwa ukosefu wa maadili katika jamii, haswa miongoni mwa vijana walio chini ya umri wa miaka kumi na nane. Lakini utapata binadamu ndio wa kulaumiwa kwa kuhusika na upotovu. Kwani katika pilka pilka zake hapa jijini nairobi, damaris kitavi alikumbana na duka moja la jumla likiuza aina ya peremende iliyo na muundo kamili wa sehemu za siri za mwanamume. La mno, ni kuwa peremende hizi ziliwekwa katika maeneo ya kuuzia peremende za watoto