Mawimbi ya kisiasa yanaonekana yametulia baada ya hatua ya Rais Kibaki kubadili msimamo kuhusiana na uteuzi wa maafisa wakuu katika idara ya mahakama. Kila upande ulikuwa umenoa silaha tayari kwa vita. Lakini utulivu huu ni wa kweli au ni wa kutufumba tu macho. Wataalam wanasema kunatokota na waliojihisi wamepata pigo katika matukio haya yote, wanapanga mikakati ya kulipiza kisasi. Katika makala ya kinyanganyiro wiki hii Munira Muhammad anachambua vita vimeelekezwa wapi kwa sasa.