Wenyeji wa Kirinyaga ya kati watapiga kura hapo kesho na kumchagua atakaye kuwa mbunge wao kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu ujao kabla ya uchaguzi mkuu. Lakini kuna maswala kadhaa amabayo yamewaathiri wenyeji wa eneo hili kwa muda mrefu ikiwemo changamoto za barabara mbovu matumizi mabaya ya fedha za mashinani maarufu kama CDF malipo duni ya wakulima wa kahawa na majani chai na pia swala nyeti kuhusiana na donda ndugu la kundi haramu la mungiki.Katika makala maalum kutoka Kirinyaga ya kati Anne Ngugi anapigia msasa maswala haya kwa kuyajadili na wenyeji wa huko.