Chama cha kanu sasa kimetaka viongozi wake wanaoshikilia nyadhifa za umma wang’atuke kutoka uongozi wa chama kama inavyohitajika kwenye katiba mpya. Uamuzi huo umefikiwa hii leo kwenye mkutano wa baraza kuu la kitaifa la chama hicho, uliofanyika katika hoteli ya Carnivore jijini Nairobi. Hatua hii imefuatia kesi iliyofunguliwa na walalamishi wa chama hicho katika mahakama ya Mombasa.