Huku dunia nzima ikisalia na mshangao kufuatia ufichuzi wa mazungumzo ya serikali ya marekani na balozi zake duniani, balozi wa Marekani Michael Ranebarger amekariri kuwa mawasiliano kati ya katibu wa Marekani kuhusu maswala ya bara Afrika Johnny Carson na waziri mkuu Raila Odinga yalikuwa tu kutayarisha nchi ya Kenya kwa stakabathi hizo wala hayakuwa ya kuomba msamaha kinyume na madai ya msemaji wa serikali Alfred Mutua. Rannerberger hata hivyo amekiri kuwa marekani inajuta sana kuhusu sakata hii ya wiki leaks.


Mtandao Wa WikiLeak