Waziri mkuu Raila Odinga ambaye pia ni kinara wa chama cha ODM amewataka wabunge waasi wa chama hicho wakiongozwa na mbunge wa Eldoret kaskazini William Ruto kukihama rasmi chama hicho badala ya kutoa vitisho na kukwaza maendeleo ya chama. alikuwa akiongea kwenye mkutano wa baraza la chama hicho katika ukumbi wa bomas.