Meya wa Nairobi Geoffrey Majiwa hii leo alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka kuambatana na ununuzi wa ardhi ya maziara katika manispaa ya mavoko. Hata hivyo Majiwa alikanusha madai dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 2.5. naibu karani wa manispaa ya thika anayedaiwa kuhusika katika kashfa hiyo ya kuilaghai serikali fedha alikwepa kufika mahakamani na kuamrishwa kufika mahakamani tarehe tisa mwezi Novemba.


Majiwa Ashtakiwa