Kongamano la wakuu wa shule limefika tamati mjini Mombasa huku walimu wakitoa msururu wa matakwa ambayo wanataka serikali itekeleze katika kuimarisha maslahi ya walimu nchini.Walimu hao kando na kutaka awamu zilizosalia za nyongeza ya mishahara kwa walimu kutekelezwa, wametoa matakwa mengine kama vile kupewa marupurupu ya burudani, kando na kutunukiwa likizo ya kugombea nyadhfa za kitaifa za kisiasa. Walimu hao vilevile waliitaka serikali kuwafadhili katika azma zao za kisiasa, hoja iliyopingwa vikali na tume ya kuwaajiri walimu TSC.


Matakwa Ya Walimu