Katika juhudi zao za kutatua mahitaji ya nguvu za umeme yanayozidi kuongezeka, huku wakiwa na ufahamu tosha kuhsuu hatma yao ya kuwa hawana umeme kutoka mtandao wa kitaifa, wakaazi wa kijiji cha kathuna katika eneo la kieni kule Nyeri; mashariki mwa mlima Kenya, wameamua kuzalisha nguvu za umeme kutokana na tufani ambayo kwa kawaida hutawala eneo hilo kila uchao .hii leo katika sehemu ya kwanza ya makala ya kawi ya upepo, ripota wetu zawadi mudibo anaangazia maisha ya mwanakijiji mmoja asiye na nguvu za umeme bomani mwake ili kuelezea ni nini hasa kilichopelekea uvumbuzi huu wa kinyumbani wa mtambo wa kuzalisha kawi ya upepo.