Rais Mwai Kibaki amesema kuwa kenya imetoa mfano mzuri kwa nchi nyinginezo haswa baada ya kuidhinisha katiba mpya. rais kibaki alikuwa akizungumza kutoka jiji la New York nchini marekani katika ufunguzi rasmi wa kikao cha umoja wa mataifa. Naye waziri mkuu Raila Odinga yumo ziarani nchini ujerumani alikokutana na wakenya nchini humo na kuwahimiza kukumbatia uraia wao kwani sasa kenya ni mpya.