Ali Chirau Mwakwere amehifadhi kiti cha ubunge katika neo la Matuga .Mwakwere aliibukaa mshindi katika hesabu ya kura baada ya uchaguzi wa hapo jana. Hata hivyo licha ya shamrashamra za upande wake, upande wa ODM wa Hassan Mwanyoha umekubali kushindwa lakini ukalimbikizia upande wa PNU lawama kwa kununua kura kando na kuwatishia wapiga kura katika ngome za wapinzani wao.