Baada ya ngoja ngoja sasa azimio la kuwa na soko huru la nchi za Afrika Mashariki litatimia kuanzia usiku wa leo. Sasa wanabiashara kutoka nchi hizi wataweza kuvuka mipaka kwa njia huru kufanya biashara na kuinua uchumi wa afrika mashariki. Hata hivyo hatua hizi zinatarajiwa kuimarishwa polepole hasa ikikumbukwa kuwa muungano wa Afrika Mashariki uliokuwepo ulivunjiliwa mbali kwasababu ya changamoto kadhaa. wengi wanasubiri kwa hamu kuona ni vipi mwingiliano huu wa kibiashara utakuwa.