Taarifa kuhusu visa vya uhalifu uliokithiri nchini kutokana na matumizi mabaya ya simu za rununu huenda sasa vikapungua kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa shughuli ya kuzisajili laini zote za simu. Serikali sasa imeamuru kuwa wenye simu za rununu kote nchini wanahitajika kuzisajili nambari zao za simu kufikia mwishoni mwa mwezi ujao. Katibu mkuu katika wizara ya mawasiliano Bitange Ndemo aliongezea kuwa, itakuwa rahisi kwa maafisa wa usalama kukabili uhalifu kote nchini iwapo laini zote za simu zitasajiliwa.


Usajili Wa Simu