Hata baada ya kuweka transfoma thelathini katika maeneo tofauti jijini Nairobi  hapo jana ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa nguvu za umeme kwa wateja wake, kampuni ya kusambaza nguvu za umeme nchini KPLC imeripoti kuharibiwa kwa transfoma kumi usiku wa kuamkia leo. Yadaiwa uharibifu huo unatokana na tamaa ya wafanyibiashara walaghai wanaoiba mafuta yapatikanayo kwenye mitambo hiyo na kuwauzia wenye magari kwa bei duni.


Wizi Wa Transfoma