Watu wawili wamefariki katika eneo la mlima Elgon na wengine watano kulazwa katika hospitali ya Bungoma kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyoathiri wakaazi wa tarafa ya Cheptais usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu na utawala wa mkoa wa magharibi,familia themanini tayari zimehamishwa na inatarajiwa watu zaidi wataondoka kutoka maeneo hayo ili kuepukana na hatari zaidi ya maporomoko.