Usitumie kila kitu [Picha: Hisani]

Kuna watu na manjumu hapa duniani.

Kuna wasee wako na kakitu na wale hawana any hapa ulimwenguni. Kuna wale raiya wenye hujua kujisundia kakitu na kuna wale hujua kutumia kakitu.

Kama sir Jah amekueka hai na hauna kakitu uskonde, uhai ni muhimu kuliko chedaz.

Kama uko hai na huna chedaz but uko salama hauna ugonjwa, ambia sir God asante umeona December ya 2016 na unaenda kukemba 2017 bila worries.

Na ukumbuke kuna wengi sana wako na pesa kuruka lakini hawajaona hii December. Kuna wale wako na kila kitu wanataka lakini hii Christmas wako hospitali, lakini wewe uko fiti uko free hata kama mfuko imetoboka.

Kuna yule mfuko imenona lakini hana freedom juu ako jela na hata kama umesota hii Christmas uskonde na uskue na mbrrr cha yoyote.

Kukosa ka kitu ni kawaida hapa Kenya, na watu wengi sana huku chini wamesota ndio maana naona badala ya Wabunge na mabigi wetu kupiga siasa za 2017 saa hizi wangekua wakipigania masafarah wapate sherehe fiti za Christmas.

Tuliwaona siku ingine wakipigana — ingekuwa wanapigananga hivyo wakijaribu kufungulia masafarah njia, basi Kenya ingekua tick.

Lakini hata kama umesota usikatsie Christmas yako, jibambe to the fullest na ile kidogo uko nayo na usiskilie wale wako na kakitu wivu halafu sir Jah atakuonekania 2017.

Kama jehova amekubariki na umekatinga, shukuru pia, na ujinice yako yote. Kitu iko ni eti usisahao wale raiya hawana kakitu — kuna watu wengi wanauliza Christmas itatoka wapi, wasaidie.

Najua huwezi saidia kila mtu juu ni wengi, but hata kama ni mmoja, give back to the society.

kuna pia children’s home, kuna orphans, kuna machokosh na watu wengine wengi wanahitaji Christmas but hawana juu wamesota. Unaweza ukawasaidia kama umekafunga — kama hujui skiza ngoma inaitwa “Give a Helping Hand (feat. Luciano and Anthony B. Ama uskize Lucky Dube ngoma inaitwa “The hand that giveth” na utakuwa mpole.