Na Carren Omae
Mvutano unatishia kuzuka katika Chama cha Ford Kenya baada ya baadhi ya wajumbe kukana madai ya kumwidhinisha kiongozi wao ambaye pia ni mmoja wa vinara wa CORD, Moses Wetangula kuwania urais wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Wakati wa kikao na wanahabari jijini Kisumu, wajumbe hao kutoka maeneo mbalimbali nchini wamempa Wetangula makataa ya siku kumi na nne kuandaa Kongamano la Kitaifa na Wajumbe kuwachagua viongozi wa chama, vilevile atakayewania urais. Ken Wafula ni Mwenyekiti wa Muda wa chama hicho.
Aidha amemshtumu kwa madai ya usimamizi mbaya wa chama huku akisema anayabagua baadhi ya maeneo huku akizingatia eneo la Magharibi pekee.
Wajumbe hao wamepinga uteuzi wa Seneta wa Kakamega, Bonny Khalwale kuwa Naibu Kiongozi wa chama wakisema uteuzi wake haukufanywa kwa njia inayofaa.
READ MORE
Fernandes equals assist record as Man Utd edge Forest thriller
Senate pokes holes in Dr Gikonyo's health findings on Gachagua
Wetang'ula tells Uhuru to act as a Statesman amid opposition criticism
Court blocks Wetang'ula from suspending MP Wamboka as PIC Chair