Waziri wa Elimu Prof. George Magoha amewataka walimu wakuu kuhakikisha wanafunzi wote wanaotarajiwa kuwa watahiniwa wa mitihani ya KCPE na KCSE 2022 wanasajiliwa kufikia tarehe 14 Mei.
Akizungumza katika Kaunti ya Kakamega, Magoha amelalamika akisema shule nyingi bado hazijawasajili watahiniwa licha ya makataa kukamilika huku akionya kwamba muda huo hautaongezwa.
Wakati uo huo, Waziri Magoha ameendelea kuwaonya walimu wakuu katika shule za upili kwa kukataa kuwaidhinisha wanafunzi ambao hawana karo.
Amewataka walimu wakuu kuwasajili wanafunzi hao kisha kutuma majina kwa Wizara ya Elimu ili kufadhiliwa chini ya mpango maalum wa serikali unaolenga kuwafadhli wanafunzi 9,000 kutoka jamii maskini na mayatima.
READ MORE
Did they have to die? Kin of fuel protests victims demand justice
Oburu moves to calm branch tensions amid UDA, Linda Mwananchi pressure
Mokaya, Moraa and Kongani shine at Mother's Day golf tournament in Kisumu
Licha ya shule kufunguliwa wiki iliyopita kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, wanafunzi wengi bado hawajaripoti shuleni huku Magoha akiahidi kuweka juhudi zaidi ili kuhakikisha kwamba sera ya 100 percent transition rate inatimizwa