Na Carren Omae
Zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kukamilika kwa mchakato wa kumwidhinisha rasmi Jaji Mkuu mteule, Jaji David Maraga, baadhi ya wakazi wa Eneo Bunge la Ainamoi wameandaa hoja mbili wanazotarajia kuwasilisha katika Bunge la Kitaifa, kupinga uteuzi huo. Hoja hizo zimetayarishwa na Emmanuel Korir anayelenga kuwania kiti cha ubunge na mwandani wa Mbunge wa Ainamoi, Benjamin Langat, Tom Biegon.
Wawili hao wanapinga uteuzi wa Maraga kwa misingi ya uamuzi wa kesi aliyotoa mwaka 2008 ambapo alipunguza mashtaka ya Andrew Omwenga kutoka yale ya mauaji hadi mashata ya kuua bila kukusudia, kwa tuhuma za kumuua aliyekuwa Mbunge wa Ainamoi, David Kimtanui Too. Wanasema uamuzi huo ulipingwa na kesi hiyo ingali katika Mahakama ya Rufaa.
Jaji Maraga anatarajiwa kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria Jumatano wiki ijayo baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuwasilisha jina lake kwa Bunge la Kitaifa.
Kulingana na Biegon, wakazi wa Ainamoi hawajakubali uteuzi huo na wanalitaka bunge kutomwidhinisha.
READ MORE
Wetang'ula tells Uhuru to act as a Statesman amid opposition criticism
Uhuru in Uganda for Museveni swearing in for a seventh term
Uhuru in Uganda for Museveni's inauguration
Why Africa's leaders cannot fix a trust crisis they helped create