Muda mfupi uliopita, nilipokea barua hii ya onyo toka kwa msomaji mmoja:

Mr Mohammed Ali, you are a young boy, apparently you just married the other day and you now have a son less than one year old. I want to give you a last warning. life is so precious if you don’t know. Leave Jubilee Regime alone. Wachana na Serikali. Wacha kuingilia Serikali. Utaumia kijana. Kama unataka kupata shida utaipata tu. Fanya kazi zako kwa makini sana. Sita kwabia tena. Kama unataka kuwa mwanasiasa jiunge na opposition, na ujue kuna conswquences. You are warned young boy. Never again oppose or criticise government. You can go to police if you wish. I can even give you my number. I am very powerful. 0721 416582.

Ninaitwa Robert Wachira.

Baada ya kusoma barua hii, ni wazi kuwa imeandikwa na mtoto wa nyoka anayetaka kuwa kama yule joka aliye watemea wakenya sumu ya ufukara na dhulma.

Nimeamua kuchambua mambo matatu kutokana na barua hii.

Kwaza, tishio lake mwandishi wa barua hii ni la kipumbavu kwani anayetaka kufanya jambo hajipigi kifua na kujiweka wazi.

Tabia yake ni sawa na mtu anayefurahia kuvalishwa maganda ya jeshi kisha kupigwa picha na kuwaonyesha marafiki zake akijitapa kuwa wakati mmoja alikuwa balaa bin belua.

Jambo la pili ni kwamba Robert ana hofu ya mwamko mpya wa wakenya wanaotaka kuiondoa serikali hii ya wanafiki. Kwa yeye kutumia chama cha Jubilee kama chambo ni njia moja ya kujificha ndani ya klabu ya wakora. Robert yumo ndani ya klabu hii.

Jambo hili si geni kwani hivi majuzi, nilitishiwa na afisa mmoja wa polisi huko Lamu, ingawa makao makuu ya polisi ilibakia tu kumkinga afisa yule. Kwa watu wa klabu hii, haki ni kunyamaza na kujifanya hamnazo.

La tatu, Robert Wachira siye mwenye ujumbe. Mwenye ujumbe ni mfuga mbwa fulani.Labda mwenye mbwa huyo ameona nguvu za wakenya kupitia mitandao; labda ameona uwezekano wa vuguvugu jipya la kuwakwamua Wakenya hivi karibuni. Swali ni, mbona Robert anipe namba yake ya simu? Ni wazi huyu ni mtoto anayeanza kubalehe.

Ni wazi kuwa kuna kikundi cha watu serikalini waliyo tayari kuzima kila aliye na sauti na ushawishi wa kupinga sera zao chafu. Wamemchagua kuizima sauti yangu kwani ninawaeleza vijana jinsi serikali ya Jubilee ilivyofeli.

Naarifiwa wao wanadhani nimelipwa na kiongozi wa Cord Raila Odinga ili kutaja maovu haya. Nafahamu fikra hofu yao kuu.

Kila mkenya, wakiwemo waislamu, wameona maovu mengi. Watoto wengi wamepotea kijambazi, wake wameachwa wajane. Dhulma dhidi ya jamii fukara zimekithiri huku Wasomali kule Eastleigh wakizidi kuteseka. Garissa an hata Mandera kumekuwa na vioja na mauji ya kila mara huku kisingizio kikiwa vita dhidi ya ugaidi. Wengi wetu wakenya tumekosa vitambulisho wala pasi za usafiri, huku polisi wakiwafanya wao kama kitega uchumi. Wakenya lazima wafanye mabadiliko 2017.

Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN. Kuwasiliana naye: mali@standardmedia.co.ke, FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali, Twitter: @mohajichopevu