Na Carren Omae
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amekana kutumia stakabadhi ghushi za masomo alipokuwa akitafuta tiketi ya uteuzi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013. Kadhalika amekana kutoa maelezo na maazimio ya uwongo kwa maafisa wa umma.
Kwa mujibu wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC, stashahada ya Sudi katika Somo la Biashara na cheti cha Shule ya Upili zilikuwa ghushi. Ameachiliwa kwa shilingi laki tatu pesa taslimu.