Na, Beatrice Maganga

Taifa linaendelea kuomboleza kifo cha mwasiasa mkongwe, William Ole Ntimama huku Rais Uhuru Kenyatta leo hii akiitembelea familia ya mwendazake kwenye Mtaa wa Lavingtone jijini Nairobi ili kuifariji. Rais ameandamana na viongozi mbalimbali serikalini wakiwamo Waziri wa Masuala ya Humu Nchini, Joseph Nkaissery.

Halfa ya mazishi ya kigogo huyo wa siasa aliyefariki dunia wiki iliyopita imeahirishwa kutoka Jumamosi hii hadi tarehe kumi na nne mwezi huu kutokana na wito wa serikali.

Kamati inayoshughulikia mazishi ya mwendazake chini ya uongozi wa Hassan Ole Kamwaro na Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Alex ole Magelo iliahirisha mazishi hayo ili kutatoa fursa kwa Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine serikalini kuhudhuria.