Ni wiki ya pili sasa, mapigano yanaendelea nchini Sudan Kusini. Zaidi ya watu 300 wamefariki
dunia. Sio raia wa taifa hilo pekee walioathirika bali wa mataifa mbalimbali. Swali langu ni je,
Sudan Kusini tatizo li wapi? Ni miaka mitano tu baada ya kujipatia uhuru kutoka Sudan, kilio
cha mwanzo kilikuwa ni unyanyasaji kutoka kwa taifa linaloongozwa na Omar al Bashir lakini
kwa mtazamo wangu ilivyo sasa yapo zaidi yanayoibua hisia baina ya wananchi na kutoelewana
kati ya rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar.
Keep Reading
- Self care: The path to being a better parent
- How to deal with sibling rivalry
- How to introduce children to budget literacy
- Modern fatherhood: Rise of the present dad
Nawazia hivi, viongozi wetu wa Afrika wakati umewadia kuweka maisha ya wananchi mbele
na kufikiria uchumi wa matiafa yetu. Sio jambo la busara kuwaona tunaowaita viongozi kuwa
ndio wa kuwapiganisha wananchi. Nina hakika mapigano hayo yanapoendelea viongozi hao
mashuhuri wana walinzi, askari waliopokea mafunzo ambao hujitolea kwa hali na mali
kuwalinda wakubwa wao, lakini wananchi je?
Wengi hujikuta katika kambi za wakimbizi hasa katika mataifa jirani, hali ya maisha katika
kambi hizo ni ngumu, wengi hufariki hata kabla ya kupata makao mbadala, nani wa kuwajali?
Kwa mfano Kenya ina wakimbizi wengi kutoka Sudan Kusini. Ingawa idadi yao ni kubwa, kuna
wengi waliosalia kuteseka nchini mwao na wengine ambao wameangamia kutokana na
makombora ya pande hasimu.
La kushangaza ni kwamba taifa hilo lina utajiri mkubwa wa raslimali, kama vile mafuta.
Viongozi hawa wangaliketi nchini na kufanya mazungumzo lingekuwa taifa
ambalo linatamaniwa kote ulimwenguni.
Anavyosema muhariri wangu ''haiwezekani kuwaweka maadui wawili wakalala pamoja, mmoja
anaweza kumuua mwezake kabla ya machweo''. Je, ndiyo hali ya Machar na Kiir? Viongozi
hawa ni maadui ambao hawawezi kuelewana kwa ajili ya taifa changa zaidi ulimwenguni? Kama
ni hivyo basi, taasisi zenye mamlaka zaidi katika ukanda huu kama vile Umoja wa Afrika,
Jumuiya ya Afrika Mashariki na mamalaka ya maendeleo katika ukanda huu, IGAD zinafaa
kuwachukulia hatua madhubuti wawili hao. Wanafaa kuwajibishwa ili warejeshe amani na
kuidumisha la sivyo waongozwe kuwapa wengine wanaojali raia fursa ya kuongoza. Kwa sababu
ukosefu wa usalama katika taifa hilo, bila shaka utayakosesha usingizi mataifa jirani Kenya
ikiwamo.
Carren Omae, Ripota Radio Maisha
omaecarren@gmail.com comae@standardmedia.co.ke
Twitter: @CallenOmae