Na, Carren Omae, Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa taifa hili. Ndio sababu Kampuni ya Maziwa ya Brookside huandaa maonesho ya kilimo kila baada ya miaka miwili ili kutoa mafunzo kwa wakulima hasa wafugaji kuhusu jinsi ya kuimarisha mapato yao. Mwaka huu, kampuni hiyo imeandaa maonesho hayo ambayo yataandaliwa mwishoni mwa mwezi huu kwa kipindi cha siku tatu.  Lengo la maonesho hayo ambayo huandaliwa kila baada ya miaka miwili na kampuni ya Brookside kwa mujibu wa Afisa wa Uhusiano mwema wa kampuni hiyo Wilson Okongo ni kutoa mafunzo kwa wafugaji, ili kuwasaidia kuimarisha mapato yao, anavyoeleza Amesema katika maonesho ya mwaka huu kutakuwa na wataalamu mbalimbali ambao watatoa mafunzo kwa wakulima kuhusu mbinu za kisasa za kupata mapato bora. Kampuni hiyo vilevile imepata ufadhili wa maonesho hayo kutoka kwa kampuni nyingine. Hadson Konji afisa wa kampuni ya Vetcare inayohusika na utengenezaji wa dawa za mifugo na ambayo ni miongoni mwa wafadhili amesema wanalenga kuwaelimisha wafugaji kuhusu umuhimu wa kuwachanja na kuwapa dawa mifugo mara kwa mara. Kampuni ya Unga Limited ambayo inahusika na utengenezaji wa chakula cha mifugo anasema kuna umuhimu wa kuwapa mifugo chakula cha kununuliwa madukani (Processed foods). William Rumooh ni afisa wa kampuni hiyo.